Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:59

Marekani : Kimbunga Ida chaongezeka kasi na kinatarajiwa kutua Louisiana


Boti, Malori na magari mengine yakiongozana katika barabara kuu ya Louisiana no 46 baada ya wamiliki wa vifaa hivyo kuvileta katika eneo ambalo liko salama wakati kimbunga Ida kikipiga katika mji wa St. Bernard Parish, Louisiana, Agosti. 28, 2021.
Boti, Malori na magari mengine yakiongozana katika barabara kuu ya Louisiana no 46 baada ya wamiliki wa vifaa hivyo kuvileta katika eneo ambalo liko salama wakati kimbunga Ida kikipiga katika mji wa St. Bernard Parish, Louisiana, Agosti. 28, 2021.

Kituo cha Taifa cha Kimbunga Marekani kimesema Jumapili kuwa kimbunga Ida kiwango cha 4 “kimeendelea kuongezeka kasi” na “ni hatari sana” wakati kikielekea kutua eneo la kusini mwa Louisiana. 

Kituo hicho kimesema ndege inayofuatilia kimbunga imeonyesha kuwa Ida kinasogea “kikiwa na kasi ya upepo wenye nguvu ya juu kabisa kufikia kilomita 230 kwa saa.”

Mapema Jumapili, Idara hiyo imeeleza kuwa Ida “kimeendelea kuongezeka kasi kwa haraka” na kilikuwa kinaenda kwa upepo wenye nguvu ya juu kabisa wa kilomita 215 kwa saa.

Ida kilitarajiwa kufika Louisiana wakati ikiwa ni miaka 16 tangu Kimbunga Katrina kutua hapo, cha kiwango cha 3 kilichosababisha vifo vya watu 1,800, vizuizi kubomoka na kuleta mafuriko yenye maangamizi huko New Orleans. Vizuizi vya maji vilivyowekwa na serikali kuu katika mji huo vimeboreshwa tangu dhoruba ya mwaka 2005.

Picha ya satellite ikionyesha kimbunga Ida katika Ghuba ya Mexico na kikielekea pwani ya Louisiana, Agosti. 29, 2021. (NOAA/Handout)
Picha ya satellite ikionyesha kimbunga Ida katika Ghuba ya Mexico na kikielekea pwani ya Louisiana, Agosti. 29, 2021. (NOAA/Handout)

“Mfumo huu utapata majaribio,” Gavana wa Louisiana John Bel Edwards amesema.

Edwards alitangaza hali ya hatari na amesema wanajeshi 5,000 wa Ulinzi wa Taifa walikuwa tayari katika ukanda wa pwani kwa ajili ya kutafuta watu na kuwaokoa. Pia wafanya kazi wengine 10,000 walikuwa tayari kukabiliana na matatizo ya umeme wakati dhoruba hiyo itakapopita.

“Hadi Jumamosi jioni, kila mtu alitakiwa kuwa katika eneo ambalo unaweza kuwa salama wakati kimbunga hicho kikipiga,” Edwards amesema.

Tahadhari ya kimbunga ilitolewa kutoka eneo karibu na Lafayette, Louisiana, hadi jimbo la Mississipi, umbali wa karibuni kilomita 320.

Tahadhari ya dhoruba pia ilitolewa eneo la Alabama-Florida, na eneo la Mobile Bay lenye maji huko Alabama pia yako katika tahadhari ya kimbunga. Gavana wa Alabama Kay Ivey pia ametangaza hali ya hatari kwa maeneo ya mwambao na kaunti za magharibi.

XS
SM
MD
LG