Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:33

Wanafunzi waliyotekwa nyara Nigeria waachiliwa huru


Wanafunzi waliyotoroshwa makwao na kundi la Boko Haram Nigeria kwenye picha ya maktaba
Wanafunzi waliyotoroshwa makwao na kundi la Boko Haram Nigeria kwenye picha ya maktaba

Watu wenye silaha wamewaachilia huru wanafunzi waliotekwa nyara miezi mitatu iliyopita kwenye shule ya Kiislamu katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Niger, wazazi wawili wameambia shirika la habari la Reuters Alhamisi.

Karibu wanafunzi 136 walitekwa nyara mwezi Mei kwenye shule katika mji wa Tegina, lakini Jumatatu, mmiliki wa shule hiyo alisema wanafunzi 6 walifariki kutokana na ugonjwa.

Afisa ambaye hakutaka jina lake litajwe amethibitisha kuachiliwa huru kwa wanafunzi hao. Mzazi mmoja aitwaye Mallam Saidu Tegina ameiambia Reuters kwa njia ya simu kwamba wanafunzi wameachiliwa huru, lakini hakusema ni wangapi.

Makundi yenye silaha ambayo yanafanya utekaji nyara ili kupata fidia, yanashutumiwa kwa msururu wa uvamizi kwenye shule kaskazini mwa Nigeria miezi ya hivi karibuni, yakiwa yameteka nyara zaidi ya wanafunzi elfu moja tangu mwezi Disemba.

Abubakar Garba Alhasan, ambaye watoto wake saba wanashikiliwa na kundi la watekaji nyara, amesema wanafunzi walikuwa njiani kuelekea mji wa Minna.

XS
SM
MD
LG