Watu 103 waliuawa, kati yao raia 90 wa Afghanistan na wanajeshi 13 wa Marekani, kulingana na Pajhwok, shirika kuu la habari la Afghanistan, na Pentagon.
Guterres ameliita shambulizi la kigaidi lililotokea wakati umati wa raia wa Afghanistan ulipokusanyika kwenye uwanja wa ndege, wakitafuta kuikimbia nchi katika siku za mwisho huku ndege zikiwahamisha watu, baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa nchi hivi karibuni.
Wakati wa mkutano huo, Dujarric aliwaambia waandishi wa habari, tukio hili linasisistiza hali sio shwari huko Afghanistan.
Pia alisema linaimarisha "azma yetu tunapoendelea kutoa msaada wa haraka kote nchini kuwaunga mkono watu wa Afghanistan."
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, alituma ujumbe wa Tweet kwamba “ akilaani vikali shambulizi la kutisha la kigaidi, na kwamba kipaumbele cha muungano huo, kinabaki kuwahamisha watu wengi kwa usalama haraka iwezekanavyo.