Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:04

Marekani yalipiza kisasi dhidi ya washirika wa kikundi cha Islamic State


FILE - Picha ilichukuliwa tarehe Januari 31, 2010, photo, ndege isiyokuwa na rubani ya Jeshi la Marekani ikiruka juu ya anga ya uwanja wa ndege wa Kandahar, kusini mwa Afghanistan, katika usiku wenye mbalamwezi.
FILE - Picha ilichukuliwa tarehe Januari 31, 2010, photo, ndege isiyokuwa na rubani ya Jeshi la Marekani ikiruka juu ya anga ya uwanja wa ndege wa Kandahar, kusini mwa Afghanistan, katika usiku wenye mbalamwezi.

Jeshi la Marekani limelipiza kisasi kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani kushambulia Ijumaa usiku eneo la washirika wa kikundi cha Islamic State cha Afghanistan maarufu kama Islamic State Khorasan, au ISIS-K.

Shambulizi hili limetokea chini ya masaa 48 baada ya mlipuko mbaya wa bomu nje ya uwanja wa ndege wa Kabul.

Shambulizi hilo la Marekani lilimlenga mtu ambaye jeshi linaamini alikuwa ndiye mhusika wa kupanga shambulizi hilo la kikatili dhidi ya Wamarekani huko Kabul.

“Shambulizi la angani la ndege hiyo iliyokuwa haina rubani lilitokea katika jimbo la Nangarhar la Afghanistan,” Kapteni Bill Urban, msemaji wa kikosi cha Marekani cha Central Command, amesema katika taarifa yake.“dalili za awali zinaonyesha tumemuua aliyekusudiwa.

Tunachojua hakuna raia aliyeuawa.” Haikujulikana hadi hivi sasa iwapo mtu aliyelengwa alikuwa amehusika na kupanga shambulizi katika uwanja wa ndege wa Kabul.

ISIS-K imedai kuhusika na mlipuko wa bomu uliosababisha maafa uliofanywa na mtu aliyejitoa muhanga katika eneo la uwanja wa ndege wa Kabul Alhamisi ambapo wananchi wa Afghanistan wasiopungua 170 na wanajeshi wa Marekani 13 waliuawa.

Watu waliojeruhiwa wakipelekwa hospitali baada ya shambulizi uwanja wa ndege wa Kabul, Kabul, Afghanistan Agosti. 26, 2021.
Watu waliojeruhiwa wakipelekwa hospitali baada ya shambulizi uwanja wa ndege wa Kabul, Kabul, Afghanistan Agosti. 26, 2021.

Siku ya Ijumaa, kwa mara nyingine tena Ubalozi wa Marekani uliwahimiza raia wa Marekani kukaa mbali na uwanja wa ndege wa Kabul kwa sababu za tishio la usalama na kuondoka mara moja iwapo wako karibu na mojawapo ya milango minne ya kuingilia uwanja wa ndege, kulingana na taarifa iliyokuwa katika tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Msemaji wa White HouseJen Psaki alisema Ijumaa kuwa maafisa wa Marekani wanafikiria kunashambulizi jingine la kigaidi ambalo “linaweza” kutokea Kabul.

Msemaji wa Pentagon John Kirby alisema katika muhtasari aliyoutowa IjumaaMarekani inaamini kuna matishio ya kweli mengine yaliyowazi dhidi ya uwanja wa ndege, akisisitiza kuwa “tuko tayari bila shaka na tunatarajia majaribio mengine siku za usoni.”

John Kirby
John Kirby

Vitisho vya usalama hivyo vimefanya zoezi la kuwaondoa Wamarekani na baadhi ya Waafghanistan kuwa gumu zaidi.

“Haionekani kama kuna juhudi za wazi zozote za kuwaondoa watu wenye visa maalum za uhamiaji, SIVs, wakati huu,” afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ameiambia VOA kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamid Karzai. Lakini wizara hiyo inaendelea kujaribu kuwaondoa raia wa Afghanistan waliokuwa wanafanya kazi ubalozini, Raia wa Marekani na wakazi wa kudumu wa Marekani.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo VOA, AP, AFP na Reuters

XS
SM
MD
LG