Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:39

Kimbunga Ida cha sababisha wakazi wa Louisiana kukosa umeme na maji safi


Mjini New Orleans wakati wa kiza kinaingia jioni huku mji wote ukiwa hauna umeme kufuatia athari za Kimbunga Ida kilicbotua Louisiana, Agosti 31, 2021.
Mjini New Orleans wakati wa kiza kinaingia jioni huku mji wote ukiwa hauna umeme kufuatia athari za Kimbunga Ida kilicbotua Louisiana, Agosti 31, 2021.

Kimbunga Ida kimewaacha mamilioni ya wakazi katika jimbo la kusini mashariki mwa Marekani, la Louisiana bila umeme na maji safi ya bomba.

Mashine nane za usambazaji umeme katika mji wa kitalii wa New Orleans, na sehemu kubwa ya kusini mwa Louisiana, ziliharibiwa wakati kimbunga Ida kilipotua hapo Jumapili.

Pia ukanda wa pwani kwenye jimbo hilo ulikuwa na upepo wa kasi ya kilomita 240 kwa saa, ulioangusha mnara mmoja wa umeme na kuingia kwenye mto Mississippi.

Mamlaka ya serikali katika jimbo na kampuni ya umeme ya Entergy kwenye eneo hilo, walisema inaweza kuchukua muda mrefu hadi siku 30, kabla umeme haujarejeshwa kikamilifu.

Taarifa hiyo imezusha wasiwasi kwamba wakazi wasio na viyoyozi huenda wakaugua kutokana na hali ya joto la eneo hilo katika kipindi hiki cha majira ya joto kali, ambapo watabiri wa hali ya hewa wanasema inaweza kupanda kati ya nyuzi 32 na 37 Celsius.

Shule zimefungwa kwa muda usiojulikana, wakati hospitali nyingi ambazo tayari zimejaa wagonjwa wa COVID-19, zinafanya kazi kwa kutumia jenereta za umeme wa dharura.

XS
SM
MD
LG