Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:30

EU yaiweka Marekani kwenye orodha hatari kutokana na Covid-19


Bendera ya Macedonia pamoja na ya EU
Bendera ya Macedonia pamoja na ya EU

Umoja wa Ulaya Jumatatu umeiondoa Marekani kwenye orodha ya mataifa salama ya kutembelea, huku ukipendekeza kurejeshwa kwa kanuni za awali dhidi ya wageni kutoka Marekani, ambako kesi mpya za maambukizi ya corona zimeongezeka katika wiki za karibuni. 

Kanuni hizo ambazo zinashauri dhidi ya kutofanya safari zisizo muhimu zimetangazwa miezi miwili tu baada ya EU kuziondoa, ingawa Marekani muda wote huu imeweka kanuni dhidi ya wasafiri kutoka Ulaya kutokana na janga la corona.

Ili taifa liwe kwenye orodha salama ya EU,ni lazima liwe na chini ya maambukizi mapya 75 kwa kila wakazi laki moja ndani ya kipindi cha wiki mbili. Takwimu za hivi karibuni kutoka CDC, zinaonyesha kwamba kuna zaidi ya maambukizi mapya 300 kwa kila wakazi laki moja ndani ya kipindi cha siku 14 hapa Marekani.

Baadhi ya mataifa mengine yaliyo ondolewa kwenye orodha salama ya EU ni pamoja na Israel,Kosovo,Lebanon,Montenegro na Macedonia Kaskazini. Baadhi ya mataifa salama kwenye orodha hiyo ni pamoja na Canada, Japan na New Zealand.

XS
SM
MD
LG