Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 04:08

Russia yaipatia Mali silaha kuendeleza mapambano dhidi ya ugaidi


Rais Vladimir Putin
Rais Vladimir Putin

Waziri wa Ulinzi wa Mali, Sadio Camara, amesema nchi yake imepokea helikopta nne, silaha, na risasi kutoka Russia Alhamisi jioni ambapo vifaa hivyo vilishushwa na ndege ya mizigo.

Amesema Mali imenunua helikopta hizo katika mkataba uliopitishwa Disemba 2020 ili kuongeza nguvu kwa vikosi vya ulinzi na usalama katika mapambano yanayofanyika kwa kushirikiana na vikosi vya Ufaransa, Ulaya, na Umoja wa Mataifa dhidi ya wanamgambo wenye uhusiano na Islamic State, pamoja na al-Qaeda.

Vifaa hivyo vimewasili wakati kukiwa na wasiwasi wa uhusiano baina ya Mali, na mshirika wake muhimu wa kijeshi Ufaransa, kuhusiana na ripoti kwamba Bamako inataka kuishirikisha Russia katika harakati hizo, wakati tayari Paris imeshapeleka kikosi maalumu cha kukabiliana na ugaidi katika eneo hilo.

Vyanzo vya Reuters vya kidiplomasiama na usalama vimeeleza utawala wa mapinduzi ya kijeshi wenye mwaka mmoja mpaka sasa upo mbioni kuajiri kundi la Russia la Wagner, huku Ufaransa ikiwa imeanzisha kampeni ya kidiplomasia kuzuia hilo, kwa kusema makubaliano hayo yanakwenda kinyume na uwepo wa Ufaransa katika eneo hilo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters

XS
SM
MD
LG