Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 07, 2025 Local time: 18:49

Mali huenda ikasogeza mbele uchaguzi wa rais na wabunge

Waziri mkuu wa mpito wa Mali Choguel Maiga, alipozungumza na waandishi mjini Bamako, Mail, May 28 2021.
Waziri mkuu wa mpito wa Mali Choguel Maiga, alipozungumza na waandishi mjini Bamako, Mail, May 28 2021.

Mali inaweza kusogeza mbele  uchaguzi wa rais na wabunge kutoka mwishoni mwa Februari ili kuzuia uhalali wake kupingwa, waziri mkuu  anayeshughulikia mabadiliko ya baada ya mapinduzi alisema.

Mali inaweza kusogeza mbele uchaguzi wa rais na wabunge kutoka mwishoni mwa Februari ili kuzuia uhalali wake kupingwa, waziri mkuu anayeshughulikia mabadiliko ya baada ya mapinduzi alisema.

Hatua ya Mali kurudi kwenye demokrasia kufuatia kupinduliwa kwa Rais Ibrahim Boubacar Keita mnamo Agosti 2020 inafuatiliwa kwa karibu katika eneo ambalo limepata mapinduzi manne katika miezi 13, mawili kati yao huko Mali.

Chini ya shinikizo kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), ambao ni umoja wa kikanda, viongozi wapya wa jeshi la Mali walikubaliana kipindi cha mpito cha miezi 18 ambacho kitahitimishwa na uchaguzi wa rais na wabunge Februari 27, 2022.

Lakini katika mahojiano na Radio France International na France24 Jumapili, waziri mkuu wa mpito wa Mali, Choguel Maiga, alisema tarehe hiyo inaweza kuahirishwa kwa wiki mbili, miezi miwili, miezi michache.

Kalenda ya uchaguz ilizingatia mahitaji ya ECOWAS bila kuangalia ni hatua gani za lazima zichukuliwe kufikia hapo, Maiga alisema. Jambo kuu kwetu si lazima iwe Februari 27 kuliko kufanya uchaguzi ambao hautashindaniwa.

Maiga alisema tarehe ya mwisho itaamuliwa mwishoni mwa Oktoba.

XS
SM
MD
LG