Ripoti kutoka shirika hilo imesema ghasia katika mkoa wa Tillaberi unaopakana na mali na Burkina Faso zimesababisha matokeo mabaya.
Zaidi ya raia 500 wamekufa kati ya Januari mosi na Julai 29 mwaka 2021, kutokana na ghasia kwenye mkoa huo.
Pia inaonyesha idadi iliyovuka mauaji ya watu 397 mwaka 2020, ripoti hiyo imeongeza kusema.
Zaidi ya watoto 60 wameuwawa na makundi yenye silaha katika maeneo ya mpakani.
Amnesty international imesema kundi moja la jihad linalohusishwa na al-Qaida –JNIM limeongeza juhudi zake kuandikisha vijana katika kundi lake.
Mamia ya shule katika mkoa huo wa Tillaberi zimefungwa kutokana na ghasia.
Ripoti hiyo imeshutumu vikosi vya usalama vya Niger kwa kushindwa kuwalinda raia lakini pia kutenda ukiukaji mkubwa.