Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:07

Mahakama ya Juu Afrika Kusini yathibitisha tena kifungo cha Zuma


Rais wa zamani Jacob Zuma
Rais wa zamani Jacob Zuma

Mahakama ya Juu nchini Afrika Kusini, Ijumaa ilithibitisha tena amri yake ya kumfunga jela Jacob Zuma.

Mahakama hiyo imemtuhumu rais huyo wa zamani kwa mashtaka ya ujanja, katika uamuzi ambao ulimtia hatiani kwa kuhujumu mahakama.

Kesi hiyo hata hivyo haiathiri kuachiliwa kwa muda Zuma, mapema mwezi huu kwa ajili ya suala la afya, jambo ambalo lilizusha malalamiko wakati wa madai ya ukiukwaji wa taratibu za msamaha.

Kifungo chake hapo mwezi Julai, kilizua mlipuko mbaya zaidi wa kisiasa tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi, wakati wafuasi wake walipofanya maandamano ya vurugu ambayo yalisababisha uporaji mkubwa wa mali katika maduka makubwa pamoja na maghala.

Zuma mwenye umri wa miaka 79, aliiomba mahakama ya kikatiba kutengua uamuzi wake wa kumhukumu kifungo cha miezi 15 kwa kukataa kujibu maswali katika uchunguzi wa ufisadi.

XS
SM
MD
LG