Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:18

Rais Ramaphosa aonya juu ya raia kujichukulia sheria


Mwanajeshi mwenye silaha akilinda doria wakati Waziri wa Jeshi la polisi Bheki Cele akizuru Phoenix, eneo jirani lililokumbwa na machafuko na mzozo wa ubaguzi karibu na Durban, Afrika Kusini, Jumamosi, Julai 17, 2021.
Mwanajeshi mwenye silaha akilinda doria wakati Waziri wa Jeshi la polisi Bheki Cele akizuru Phoenix, eneo jirani lililokumbwa na machafuko na mzozo wa ubaguzi karibu na Durban, Afrika Kusini, Jumamosi, Julai 17, 2021.

Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa, Jumapili alitarajiwa kujiunga na juhudi za kufanya usafi baada ya ghasia, wakati serikali yake ikionya dhidi ya watu kujichukulia sheria ili kuepuka mzozo wa kibaguzi kufuatia ghasia.

Rais Ramaphosa ameahidi kurejesha hali ya utulivu baada ya ghasia hizo nchini Afrika Kusini.

Nchi hiyo ilikumbwa kwa zaidi ya wiki moja ya machafuko ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 200 hadi sasa, wakati waporaji walipovamia vituo vya biashara, na makundi yasiyojulikana yakiteketeza miundo mbinu na kufunga njia za biashara.

Vurugu hizo zilikuwa mbaya sana nchini Afrika Kusini baada ya ubaguzi wa rangi, na zilizuka baada ya Rais wa zamani nchini humo Jacob Zuma, kuhukumiwa miezi 15 gerezani, kwa kuidharau mahakama kutoa ushahidi wake kuhusiana na uchunguzi wa ufisadi.

Kesi yake hiyo ni tofauti na kesi inayotarajiwa kuanza tena kesho Jumatatu.

Kadhalika Rais Ramaphosa anazidi kupata shinikizo kutokana na mshukiwa mmoja pekee kukamatwa, kati ya washukiwa wakuu wa kile maafisa wanakiita, jaribio la uasi, ambalo lilisababisha takribani dola bilioni moja za uharibifu.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali.

XS
SM
MD
LG