Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:27

Zimbabwe kutoa chanjo milioni moja ndani ya wiki mbili


Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kwenye picha ya awali
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kwenye picha ya awali

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema Jumanne kwamba serikali yake inalenga kutoa chanjo za covid 19 kwa watu milioni moja katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Kiongozi huyo pia ameongeza muda wa kufungwa kwa shughuli za kawaida kwa siku 14 zaidi. Kutokana na ongezeko jipya la maambukizi ya virusi corona pamoja na vifo nchini humo, Mnangagwa hapo Juni 29, aliweka kanuni mpya kali zikiwemo amri ya kutotoka nje nyakati za usiku pamoja na kuzuia usafiri kati ya miji.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Mnangagwa amesema kuwa maambukizi ya corona yanaongozeka kwa kasi kutokana na aina mpya ya virusi vya delta. Amesema wanalenga kutoa chanjo kwa watu milioni moja kabla ya kufunguliwa tena kwa shughuli za kawaida.

Kufikia sasa, taifa hilo la kusini mwa Afrika limeshuhudia maambukizi zaidi ya 70,000, robo yake yakiwa yametokea katika muda wa wiki mbili zilizopita. Vifo 2,236 pia vimeshuhudiwa katika muda huo. Tangu zoezi la utoaji chanjo za covid lilipoanza nchini humo, ni watu takriban 900,000 waliopata kufikia sasa.

Wiki iliyopita, Mnangagwa kupitia hotuba kwa njia ya televisheni alisema kuwa ripoti iliyotolewa wiki iliyopita inasema kuwa asilimia 80 ya maambukizi mapya ya corona ni kutokana na virusi vipya vya delta. Wiki moja iliyopita, taifa hilo lilipata kasha kubwa zaidi la dozi milioni 2 za covid wakati nyingine milioni 3.5 zikitarajiwa mwishoni mwa mwezi huu.

XS
SM
MD
LG