Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:00

Zuma apewa ruhusa ya kutoka gerezani kwa siku moja


Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma akitokea mahakamani kwa njia ya video.
Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma akitokea mahakamani kwa njia ya video.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa likizo ya huruma kwa siku moja kuhudhuria mazishi ya mdogo wake

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, akiwa gerezani kwa kuidharau mahakama amepewa likizo ya huruma kwa siku moja kuhudhuria mazishi ya mdogo wake Alhamisi, maafisa wa magereza walisema.

Zuma amefungwa katika gereza la Estcourt tangu alipojisalimisha kwa maafisa Julai 7 kutumikia kifungo cha miezi 15. Gereza hilo liko karibu na nyumba yake ya kijijini huko Nkandla katika jimbo la Kwa-Zulu Natal ambapo shughuli za mazishi zinatarajiwa kufanyika.

Kama mfungwa wa muda mfupi, aliye na hatari ndogo, ombi la Bw. Zuma la likizo ya huruma lilishughulikiwa na kupitishwa, idara ya Magereza ilisema katika taarifa, na kuongeza kuwa wakati atakapokuwa nje ya gereza hilo , Zuma hatahitajika kuvaa sare za wahalifu.

Zuma, mwenye umri wa miaka 79, alihukumiwa mwishoni mwa mwezi uliopita kwa kukaidi agizo la mahakama ya kikatiba la kutoa ushahidi katika uchunguzi wa ufisadi wa kiwango cha juu katika kipindi cha miaka yake tisa madarakani hadi 2018.

Chanzo cha Habari : Reuters

XS
SM
MD
LG