Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:05

Ramaphosa afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri


Rais wa Africa Kusini Cyril Ramaphosa akiandamana na maafisa wa serikali kwnye picha ya awali
Rais wa Africa Kusini Cyril Ramaphosa akiandamana na maafisa wa serikali kwnye picha ya awali

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa Alhamis ametaua mwenyekiti wa benki ya maendeleo ya Afrika kusini Enoch Godongwana kuwa waziri wa fedha akichukua nafasi ya Tito Mboweni baada ya kufanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Mboweni alikuwa ameomba kuacha wadhifa huo. Ramaphosa ambaye alichukua madaraka mwaka wa 2018 ameapa kuimarisha uchumi ili kuvutia wawekezaji wakati akikabiliana na ufisadi.

Mabadiliko kwenye baraza la mawaziri yameathiri mawaziri wengine 9 pamoja na naibu waziri 11. Ramaphosa amesema kuwa amefanya marekebisho hayo ili kuharakisha uwezo wa serikali wa kutoa chanjo za covid-19, kufufua uchumi na kuhakikisha udhabiti baada ya ghasi zilizo shuhudiwa hivi karibuni baada ya kufungwa kwa aliyekuwa rais wa zamani Jacob Zuma.


XS
SM
MD
LG