Msemaji wa ubalozi wa Marekani nchini Russia amesema kwamba Burns anaandamana na viongozi wengine wa ngazi ya juu kwenye ziara hiyo inayomalizika leo, baada ya kuombwa kufanya hivyo na rais Joe Biden.
Baraza la usalama la Russia limesema kwamba Burns ambaye anazungumza ki Russia, na ambaye pia alikuwa wakati mmoja balozi wa Marekani mjini Moscow, amefanya kiako na katibu wa baraza hilo, Nikolai Patrushev pamoja na aliyekuwa kiongozi wa idara ya kijasusi ya Russia ya FSB. Hakuna upande uliotoa maelezo zaidi kuhusu vikao hivyo ingawa masuala ya kiusalama yanakisiwa kutawala kwenye mazungumzo yao.
Katika siku za karibuni, Marekani na Russia wametofautiana kuhusu madai ya mashambulizi ya kimitandao dhidi ya Marekani, uungaji mkono wa Russia kwa rais wa Syria Bashar al Assad, kufungwa jela kwa kiongozi wa upinzani Alexey Navalny pamoja na mwenendo wa Russia dhidi ya Ukraine, ambako ilijinyakulia Peninsula ya Crimea mwaka wa 2014.