Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 11:35

Waandishi wa habari Msumbiji wanavyopambana taarifa za uongo


Waandishi wa habari Msumbiji wanavyopambana taarifa za uongo
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:02 0:00

Msumbiji ambako kuenea taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kunawalazimu waandishi wa habari nchini humo kuwa mstari wa mbele katika kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo .

Hapa katika chumba cha habari cha Evidencias, mjini Maputo, Msumbiji, Reginaldo Tchambule na timu yake wanafanya kazi ya kuweka rekodi sawa katika jitihada za kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo. ⁣ ⁣ Yeye na mwenzake Nelson Mucandze, wanasema walianzisha pamoja gazeti na lile la mtandaoni miaka minne iliyopita kwa sababu mashirika mengine mengi hayakuwa yakikagua ukweli au kutumia taarifa na uchambuzi katika kuripoti kwao. Tchambule anasema hadhira yao ilianza kufuatilia kwa haraka.⁣ Reginaldo Tchambule, Evidencias Editor anaeleza: “Gazeti la Evidencias linaweza kuwa limepata muonekano na umaarufu mkubwa katika muda mfupi, kwa sababu ya jinsi tulivyozingatia uandishi wa habari wenyewe. Wakati fulani tulikuwa na ukurasa ambapo tulichunguza habari kuu zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.” ⁣ ⁣ Mwaka huu, Tchambule aliripoti kwa nini Ossufo Momade, kiongozi wa Renamo, chama kikuu cha upinzani cha Msumbiji, hajaonekana hadharani kwa wiki kadhaa wakati wa kampeni za urais. ⁣ Evidencias ilianza kuchunguza picha kwenye mtandao wa Facebook wa mgombea ambapo ilionekana Momade alikuwa akifanya kazi nje ya nchi. ⁣ ⁣ Ripoti ya Amarilis Gule VOA Maputo.⁣

Forum

Makundi

XS
SM
MD
LG