Waandamanaji wakibeba bendera ya Belarus ya rangi ya nyekundu na nyeupe waliandamana hadi uwanja wa uhuru kufuatia wito wa viongozi wa upinzani kuwataka kuendekea na shinikizo la kumtaka rais kuachia madaraka.
Lukashenko aliyeko madarakani tangu mwaka 1994 akiongoza utawala wa mabavu aliwatuma kikosi chake cha kupambana na ghasia kuyatawanya maandamano yalioanza baada ya kiongozi huyo kudai ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa Ogusti 9 na kumwezesha kubaki madarakani kwa mhula wa sita.
Wizara ya ulinzi imesema itaingilia kati kukomesha maandamano kulinda majengo ya makumbusho na ya serikali. Maandamano ya kuwaunga mkono wananchi wa Belarus yanafanyika katika nchi 26, Ikiwa ni pamoja na Lithuania ambako watu wanashikana mkono na kujipanga hadi kufika mpaka wa Belarus.