Ujumbe wa ECOWAS pia utakutana na rais aliyeondolewa madarakani, Keita, pamoja na maafisa wa serikali na jeshi wanaozuiliwa na wanajeshi waasi, afisa mmoja wa ECOWAS ameliambia Shirika la Habari la AFP.
Viongozi hao watakutana na mabalozi wa mataifa matano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wanaotarajiwa kuwasili Bamako siku ya Jumapili.
Ujumbe huo umewasili siku moja baada ya maelfu ya wananchi kumiminika katika mji mkuu wa Mali wakionyesha kuunga mkono baraza hilo la jeshi liliofanya mapinduzi.
Waandamanaji huko Bamako – wengine wakinyanyua mabango yao wakipaza sauti kuwa Kamati ya Kitaifa ni Mkombozi wa Wananchi, CNSP, ni jina ililopewa baraza la utawala wa kijeshi.
Waandamanaji vile vile wanapinga ECOWAS kwa tamko lao la kulaani mapinduzi hayo na kwa kufunga mipaka ya majirani wa nchi ya Mali katika umoja wa eneo lenye nchi 14 wanachama.
Viongozi wa kijeshi waliofanya mapinduzi wamesema Ijumaa wamefungua mipaka kwa safari za anga na ardhini.