Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:28

Wanajeshi waloasi Mali wadai wanamshikilia Rais Ibrahim Boubacar Keita


Imam Mahmoud Dicko akiwahutubia wafuasi wa upinzani mjini Bamako. June 19, 2020
Imam Mahmoud Dicko akiwahutubia wafuasi wa upinzani mjini Bamako. June 19, 2020

Kundi la wanajeshi wa Mali waloingia katika mji mkuu Bamako Jumanne mchana wakifyetua risasi hewani wanasema wanamshikilia Rais Keita na baadhi ya maafisa waandamizi wa serikali yake.

Wafuasi wa upinzani walijitokeza barabarani kuwashangilia wanajeshi hao na wengine wakikusanyika kwenye uwanja wa Uhuru baada ya kupata habari kwamba, kuna wanajeshi waloasi ili kuupinga utawala wa rais Ibrahim Boubacar Keta, anaefahamika kama IBK.

Mmoja kati ya viongozi wa wanajeshi walioasi amewambia waandihsi habari kwamba wamewakamata maafisa waandamizi wa jeshi pia katika kambi ya Kati na wamechoshwa na utawala wa IBK.

Rais Emmanuel Macron, wa Ufaransa, taifa la zamani la kikoloni, amekua na mazungumzo na viongozi wa nchi za Afrika Magharibi, akihimiza kuwepo na majadiliano zaidi ya upatanishi kupitia Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), kulingana na ikulu ya Paris.

Akizungumza na waandishi habari, afisa mmoja wa wizara ya mambo ya ndani ya Mali amesema "maafisa waandamizi wanakamatwa, kuna hali ya sintofahamu, hatujui kinachotendeka."

Inaripotiwa kamba wafanyakazi wa serikali walianza kukimbia kutoka afisi zao mjini Bamako, pale watu walova nguo za kijeshi kuingia katika afisi hizo na kuwakamata Marfisa wa serikali akiwemo waziri wa fedha Abdoulaye Daffe.

Tangu mwezi June Rais IBK amekabiliwa na maandamano ya kumtaka ajiuzulu kutokana na ulaji rushwa ulokithiri na kushindwa kupambana na wanamgambo wa kislamu kaskazini mwa nchi.

XS
SM
MD
LG