Katika taarifa yake Jumatano, Ramaphosa alitaka wanajeshi waasi katika taifa hilo la Afrika Magharibi kumwachilia huru Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, Waziri Mkuu Boubou Cisse na viongozi wengine wa juu wa serikali.
Wakati wa hotuba yake ya kujiuzulu, Keita, anayeshikiliwa katika kambi ya kijeshi karibu na mji mkuu, Bamako, alitangaza kufutwa kwa Bunge la taifa na serikali ya Waziri Mkuu Boubou Cisse.
Askari, wanaojiita Kamati ya Kitaifa ya kuokoa Wananchi, walikuwa bado wakimshikilia Keita Jumatano.
Kufikia sasa, kundi hilo limesema tu kwamba litafanya kazi kuelekea uchaguzi.