Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:28

Shirika la kutetea haki za binadamu la THRDC lasitisha shughuli zake Tanzania.


Polisi wa Tanzania.
Polisi wa Tanzania.

Shirika la kutetea haki za binadamu Tanzania (THRDC), limesitisha  shughuli zake  nchini humo wakielezea  vitisho vikali na kuingiliwa katika shughuli zake na idara za  usalama nchini humo.

Uwamuzi huo umechukuliwa wiki chache tu baada ya tume ya uchaguzi ya Tanzania, kulizuia shirika hilo kutoka kwenye orodha ya mashirika yaliyoidhinishwa kutoa elimu kwa mpiga kura, na kufuatilia uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 28 nchini humo.

Tanzania imeshuhudia kushuka kwa uhuru wa msingi wa kushiriki katika masuala mbali mbali Pamoja na uhuru wa kujieleza katika miaka minne iliyopita tangu Rais John Magufuli alipoingia madarakani, na hivyo kuathiri vyombo vya habari na asasi za kiraia.

Mamlaka zilipitisha sheria kadhaa zinazokandamiza ripoti huru na zinazuia kazi ya vyombo vya habari, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na makundi vya upinzani wa kisiasa.

Vicky Ntetema, mwenyekiti wa bodi ya THRDC alisema katika taarifa yake kwamba polisi walilazimisha viongozi wa benki kufungia akaunti zao.

Kulingana na mratibu wa kitaifa wa THRDC, Onesmo Ole Ngurumwa, aliitwa na polisi Jumatatu kwa ajili ya kuhojiwa, na hivyo kuelezea ni kwa nini NGOs zilishindwa kutii wito wa serikali kuwasilisha makubaliano yake ya mikataba na wafadhili wa kigeni kama inavyotakiwa na sheria.

"Alikamatwa kwa muda mfupi na kuachiliwa baadaye kwa dhamana baada ya watumishi wawili wa umma kusaini dhamana ya shilingi milioni 200 za kitanzania," Ntetema alisema.

Kusimamishwa huko kwa THRDC ni ushahidi mwingine wa kushambuliwa kwa nafasi ya raia, alisema Zitto Kabwe, kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo alipozungumza na mtandao wa Anadolu Agency.

XS
SM
MD
LG