Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:41

Kamala Harris akubali uteuzi kuwa mgombea mwenza wa Chama cha Democratic


Kamala Harris
Kamala Harris

Ghasia za bunduki, mabadiliko ya hali ya hewa na Covid 19 ni masuala ambayo yamepewa umuhimu katika siku ya tatu ya mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Democratic jana Jumatano, wakati Seneta Kamala Harris wa California alipokubali uteuzi wa kuwa mgombea mwenza wa Joe Biden.

Tukio hilo ambalo limefanya kwa njia ya mtandao kwasababu ya janga la Covid 19, liliwajumuisha wanachama wa Democratic na wafuasi wao kutoka kote Marekani.

Ni mkutano usio wa kawaida, amesema muongozaji wa mkutano huo Kerry Washington, mcheza filamu wa Holywood.

Chumba kinachosimamia matangazo ya mtandaoni ya mkutano wa chama cha Democratic
Chumba kinachosimamia matangazo ya mtandaoni ya mkutano wa chama cha Democratic

Na katika tukio hapo jana, mwanamke wa kwanza mweusi na mmarekani mwenye asili ya Asia Kusini ambaye yuko katika tiketi ya chama kwa nafasi ya juu ya uongozi Kamala Harris alihutubia kukubali uteuzi wa chama.

Kamala Harris :“Nakubali uteuzi wa kuwa makamu rais wa Marekani.”

Mgombea Joe Biden alionyeshwa katika kanda za video, akiungwa mkono, miongoni mwa watu wengine na Gabby Giffords, mbunge wa zamani wa baraza la wawakilishi ambaye aliwahi kukumbwa na shambulizi la bunduki.

Gabby Giffords, Mwakilishi wa zamani anatema : “Marekani inahitaji sisi sote tuzungumze, hata kama unajitahidi kupata maneno ya kusema.”

Rais Donald Trump alikosolewa kwa kuimarisha sheria kali za uhamiaji na jinsi wanavyotendewa watu wanaoomba hifadhi na wahamiaji wasio na nyaraka halali.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Aliyekuwa anawania uteuzi wa kugombea urais Elizabeth Warren alikosoa jinsi rais alivyoshughulikia janga la virusi vya corona.

Seneta Warren alisema :“Leo, Marekani ina vifo vingi zaidi vinavyotokana na covid hapa duniani na uchumi umeanguka, na mizozo yote miwili ni migumu sana kwa watu weusi na familia ambazo si za wazungu.”

Rais wa zamani, Barack Obama amesema Trump haheshimu mabadiliko katika nchi au umuhimu wa kazi yake.

Barack Obama
Barack Obama

Obama alisema : “Nilikuwa na matumaini kwa ajili ya nchi yetu kwamba Donald Trump huend akaonyesha mtizamo kiasi katika kulichukulia suala la ajira kwa dhati, kwamba huenda angeweza kuhisi uzito wa kazi yake na kubaini kuwa demokrasia iko katika mikono yake hivyo achukue hatua zinazostahili. Lakini hajawahi kufanya hivyo.”

Aliyewahi kuwa mgombea wa Democratic kwa nafasi ya rais, Hillary Clinton amesisitiza umuhimu wa kupiga kura.

“Kumbukeni mwaka 2016 wakati Trump alipoulizwa,”una kitu gani cha kupoteza?’, ndiyo, hivi sasa tunalifahamu hilo. Huduma zetu za afya, kazi zetu, wapendwa wetu,” Clinton alieleza.

Amesema kuwa kuwafikia wapiga kura katika mwaka 2020 ambako kuna janga la Covid 19 nalo ni muhimu.

XS
SM
MD
LG