Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:38

Marekani yawawekea Waganda 4 vikwazo kwa ulaghai wa malezi ya watoto


Mabara ambayo Sheria ya Kimataifa ya Uwajibikaji wa Haki za Binadamu ya Magnitsky inatumika.
Mabara ambayo Sheria ya Kimataifa ya Uwajibikaji wa Haki za Binadamu ya Magnitsky inatumika.

Wizara ya Fedha ya Marekani inayodhibiti Mali za Marekani Nje ya Nchi (OFAC) imewawekea vikwazo raia wanne wa Uganda kufuatia amri ya kiutendaji nambari 13818 inayoimarisha na kutekeleza Sheria ya Kimataifa ya Uwajibikaji wa Haki za Binadamu ya Magnitsky.

Watu hawa wameadhibiwa kwa kujihusisha na ulaghai wa malezi ya watoto ambao umeshuhudia watoto waliozaliwa Uganda wakikabiliwa na madhila katika mikono ya waliokuwa wanaendesha mradi huu.

“Kuwadanganya familia za Waganda wanaotii sheria kuwa wawatoe watoto wao kwa ajili ya kulelewa na watu wengine kumesababisha majonzi makubwa,” amesema Waziri Mdogo wa Hazina Justin G. Muzinich.

“Watu waliohusika na utapeli huu kwa makusudi waliwalaghai Waganda wenye nia nzuri na Wamarekani kujitajirisha wao wenyewe.

Marekani itaendelea na ahadi yake ya kuwatafuta na kuwafichua watu wote wanaokiuka haki za binadamu ulimwenguni.

Takwimu za Wizara ya Mambo ya Nje juu ya Uasili wa watoto wanaotokea Uganda kuja kulelewa Marekani katika mwaka wa 2018 (zilizoripotiwa Machi 2019) : Uganda : watoto 26 (23 taratibu zimekamilishwa nje ya nchi; 3 ilikuwa taratibu zao zikamilishwe Marekani).

Majaji Waliohusika na Utapeli

Majaji wa Uganda Moses Mukiibi (Mukiibi) na Wilson Musalu Musene (Musene), Mawakili Dorah Mirembe (Mirembe), na mumewe Mirembe, Patrick Ecobu (Ecobu), walishiriki katika utapeli huo ambao katika mazingira fulani, watoto waliondolewa kutoka kwenye familia zao Uganda kwa ahadi ya programu maalum “kupatiwa elimu” na kusoma Marekani, na hatimaye wakatolewa kwa familia za Marekani kuwalea.

Matokeo yake hatua ya Jumatatu, ilihusu mali zote na maslahi yoyote katika mali zao watu hao waliotajwa katika vikwazo hivyo na kitu chochote chao wanachomiliki wao wenyewe au watu wengine, iwe ni asilimia 50 au zaidi wao wenyewe, mmoja mmoja, au na watu waliowekewa vikwazo, ambazo ziko Marekani au zinamilikiwa au kusimamiwa na watu wa Marekani, zimezuiliwa na lazima ziripotiwe katika ofisi ya OFAC.

Kampuni ya mawakili

Kampuni iliyoandaa mpango huo wa kitapeli wa malezi ya watoto hao ilitumia kampuni ya mawakili ya Mirembe kushughulikia masuala ya kisheria ya Malezi ya watoto hao, baadhi ya mipango hiyo ilikuwa ya kurubuni au kughushi nyaraka za mahakama.

Zaidi ya hilo, kampuni ya mawakili ya Mirembe wakati mwingine ilikuwa inaajiri au kutumia huduma za watu wa kati kutafuta familia zenye matatizo maeneo ya vijijini nchini Uganda kuwarubuni wazazi – ambao aghlabu hawajui kusoma au kuandika kiingereza – kutoa watoto wao kwa ajili ya kulelewa kwa kutumia ulaghai.

Kampuni ya mawakili, kwa njia ya moja kwa moja au kupitia madalali, iliwaahidi wazazi kuwa watoto wao wataletwa Kampala, Uganda, na watalelewa na wamishionari wakati wakipatiwa elimu.

Nyumba isiyokuwa na leseni

Walipoondolewa kutoka kwenye makazi yao, wengi wa watoto hao waliwekwa katika nyumba iliyokuwa haina leseni ya kulea watoto mjini Kampala, na wengi walifikishwa mahakamani na kutambulishwa kama kwamba wao ni yatima.

Wamarekani waliokuwa ndio walezi wa watoto hao bila ya kujua hilo waliwasili Uganda kuwachukua watoto hao ili kuwalea na kusafiri nao kuja Marekani.

Waliopokea Hongo

Ili kufanya mipango ya ulezi wa watoto hao, Mirembe, akisaidiwa na Ecobu, waliwahonga majaji wa Uganda Mukiibi, Musene na maafisa wengine wa serikali, moja kwa moja au kupitia kwa wakala wao.

Mirembe alikuwa amefanya mazungumzo na Musene na kukubaliana malipo ya wastani kwa ajili ya kuandaa utaratibu wa kisheria wa watoto hao kuchukuliwa kulelewa. Angalau mara moja Mirembe alikutana ana kwa ana na Musene kuandaa malipo ya ziada yaliyohitajika ili Musene aweze kuharakisha tarehe ya kusikilizwa shauri la Malezi moja lililokuwa linasubiri kushughulikiwa katika tarehe za kusikilizwa kesi inayoendeshswa na Musene.

Kufuatia kuhamishwa kwa Musene katika kitengo cha mahakama nyingine, Mirembe alifanya mpango kesi hizo zipelekwe kwa Mukiibi, ambapo angalau mtu moja alilipa hongo ya pesa taslimu kwa kuelekezwa na Mirembe.

XS
SM
MD
LG