Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:27

Robert Trump, mdogo wake Rais wa Marekani, aaga Dunia


Picha hii imepigwa Novemba 9, 2016, Rais mteule wa Chama cha Republikan Donald Trump akimkubmbatia mdogo wake Robert Trump baada ya kutoa hotuba ya kukubali kupeperusha bendera ya chama hicho New York, Marekani.
Picha hii imepigwa Novemba 9, 2016, Rais mteule wa Chama cha Republikan Donald Trump akimkubmbatia mdogo wake Robert Trump baada ya kutoa hotuba ya kukubali kupeperusha bendera ya chama hicho New York, Marekani.

Mdogo wake Rais Donald Trump, Robert Trump, mfanyabiashara ambaye alikuwa anaishi maisha ya kawaida na wala hajabebwa na jina la familia, amefariki Jumamosi usiku baada ya kulazwa hospitali New York, Rais amesema katika tamko lake. Amefariki akiwa na umri wa miaka 71.

Rais alimtembelea ndugu yake katika hospitali ya huko New York Ijumaa baada ya maafisa wa White House kueleza alikuwa mahututi.

Nina majonzi makubwa kuwafahamisha kuwa ndugu yangu mwema, Robert, amefariki kwa amani usiku,” Donald Trump ameeleza katika taarifa yake.

“Alikuwa siyo tu mdogo wangu, bali rafiki yangu mkubwa. Tutamkumbuka sana kwa kututoka, lakini tutakutana naye tena. Kumbukumbu yake itabakia moyoni mwangu milele. Robert, nakupenda. Pumzika kwa amani.”

Mdogo wao wa mwisho kina Trump alikuwa karibu sana na rais mwenye umri wa miaka 74, mwezi Juni, alifungua kesi kwa niaba ya familia ya Trump ambayo haikufanikiwa, ikitaka kusitisha chapisho la kitabu kinachoeleza kila kitu kilichoandikwa na mpwa wa rais, Mary.

Robert Trump aliripotiwa kulazwa hospitali katika kitengo cha wagonjwa mahututi kwa siku kadhaa katika mwezi huo.

‘Ni mwanamme pekee katika maisha yangu niliyekuwa namwita ‘honey’

Wote wakiwa wafanyabiashara wa muda mrefu, Robert na Donald walikuwa wanaonekana kuwa na hulka tofauti.\

Donald Trump wakati mmoja alimuelezea mdogo wake kuwa “mtu mkimya na mtulivu kuliko yeye,” na “mwanamme pekee katika maisha yangu ambaye namwita ‘honey.’”

Robert Trump alianza maisha yake huko Wall Street akifanya kazi na mashirika ya fedha lakini baadae alijiunga na biashara ya familia, akisimamia biashara ya majumba na hoteli akiwa mtendaji wa ngazi ya juu katika taasisi ya Trump.

“Alipokuwa anafanya kazi katika taasisi ya Trump, alikuwa anajulikana kama Trump mwema,” mwandishi wa maisha ya familia, ameliambia shirika la Habari la Associated Press.

“Robert alikuwa akifuatwa na watu kuingilia kati kutatua tatizo lolote linapotokea.”

Robert Stewart Trump alizaliwa mwaka 1948, ni kitindamimba wa mmiliki wa biashara ya majumba wa New York Fred Trump aliyekuwa na watoto watano.

XS
SM
MD
LG