Waandamanaji hao wanapinga hatua ya Rais Alassane Ouattara ya kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Mtu mmoja anasemekana kuuawa kwenye maandamano hayo wakati polisi walipokuwa wakikabiliana na watu waliochoma matairi pamoja na vifaa vya mbao.
Mji wa Abidjan umeshuhudia maandamano ya hapa na pale tangu wiki iliyopita baada ya Ouattara kutangaza atashiriki kwenye uchaguzi wa Oktoba 31, 2020 licha ya upinzani kulalamika kuwa ni kinyume cha katiba.
Ouatarra kwa upande wake anasema kuwa marekebisho ya katiba yaliofanywa 2016 yanampa nafasi ya kugombea urais upya bila kuzingatia mihula miwili aliohudumu tayari.
Iwapo Ouattara, mwenye umri wa miaka 78, atashiriki zoezi hilo, basi atakutana na wagombea wengine kadhaa akiwemo aliyewahi kuwa rais Henri Konan Bedie.