Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:01

Shambulizi lauwa 16 katika hoteli Mogadishu

Wafanyakazi wa afya na raia wakiwabeba watu waliojeruhiwa wakiwasili hospitali ya Madina baada ya mlipuko katika hotel ya Elite katika fukwe ya Lido mjini Mogadishu, Somalia, Agosti 16, 2020.
Wafanyakazi wa afya na raia wakiwabeba watu waliojeruhiwa wakiwasili hospitali ya Madina baada ya mlipuko katika hotel ya Elite katika fukwe ya Lido mjini Mogadishu, Somalia, Agosti 16, 2020.

Watu 16 wameuwawa katika shambulizi la Jumapili linalosadikiwa kufanywa na kundi la Al-Shabab kwenye hoteli moja mjini Mogadishu, msemaji wa serikali Ismail Mukthar Omar amesema.

Raia 11 na washambuliaji wa 5 ndio waliouawa katika shambulizi hilo, Omar aliandika kwenye twitter.

Omar ameongeza kuwa mwajeshi moja wa serekali aliuwawa, na watu 18 walijeruhiwa.

Taarifa zinasema wanamgambo wa Al Shabab walivamia hoteli ya kifafari iliyopo katika ufukwe wa Lido, walitegua bomu la kwenye gari na baadae wakafyatua risasi wakitumia bunduki za rashasha.

Hotel hiyo inamilikiwa na Abdullahi Mohamed Nor, mbunge na waziri wa zamani wa fedha, na ilikua inatembelewa sana na maafisa wa serekali na wasomali waishio nje ya nchi.

XS
SM
MD
LG