Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:16

HABARI ZA DUNIA KWA UFUPI : Bomu la kujitoa muhanga lauwa Somalia


Maafisa wa usalama Somalia waskikagua gari iliyoteketezwa kwa mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia, Julia 13, 2020.
Maafisa wa usalama Somalia waskikagua gari iliyoteketezwa kwa mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia, Julia 13, 2020.

Mtu mmoja ameuwawa, na wengine kujeruhiwa nchini Somalia katika shambulizi la bomu la kujitoa muhanga kama alivyoeleza kamanda wa jeshi Jenerali Odowaa Yusuf Rageh.

Kundi la wanamgambo wa Al Shabaab linaaminika kufanya shambulizi hilo baada ya msafara wa jenerali kuondoka katika eneo la wizara ya ulinzi mjini Mogadishu siku ya Jumatatu ambapo Jenerali huyo alinusurika katika shambulizi hillo.

Msemaji wa jeshi la Somalia Abdiqani Ali Ashkir amesema kwamba vikosi vya ulinzi viliwafyatulia risasi na kuwaua washambuliaji kabla ya gari lililokuwa na mabomu kuegeshwa na kulipuliwa. Inaelezwa shambulizi hilo lililengwa kwa jenerali Raheh, kutokana na juhudi zake za kupambana na wanamgambo hao.

IVORY COAST YAMKUMBUKA HAYATI WAZIRI MKUU

Ivory Coast imefanya kumbukumbu katika mji mkuu Abidjan, iliyorushwa kupitia televisheni na kumpa heshima waziri mkuu Amadou Gon Coulibaly, ambaye alifariki dunia ghafla wiki iliyopita kutokana na mshtuko wa moyo.

Kifo cha Coulibaly kimetokea ikiwa ni miezi kadhaa imesalia kabla ya chama tawala kufikiria kumtangaza kuwa mgombea urais.

Rais Alassane Ouattara, ambaye aliongoza kumbukumbu hizo alimtambua waziri mkuu huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 61 kuwa mtu ambaye angerithi madaraka ya rais aliyepo madarakani.

Mpaka sasa hakuna taarifa kamili za nani atachukuwa nafasi ya Coulibaly, ambaye alikuwa akiheshimika sana.

Kadia Camara, ambaye ni waziri wa eleimu wa Ivory Coast, alimtaja Coulibaly kama mwanasiasa aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kufanya upatanishi.

WATAFITI WASEMA CHANJO YA COVID-19 INAONYESHA MATUMAINI

Watafiti wa Marekani wanasema chanjo ya virusi vya corona inayofanyiwa kazi kwa sasa imeonyesha matokeo mazuri katika kukinga virusi hivyo kwa mujibu wa uchunguzi wao unao endelea sasa.

Chango hiyo mpya imetengenezwa na kiwanda cha dawa chenye makao yake Marekani, na ilitengenezwa na watafiti kutoka taasisi ya taifa ya magonjwa ya kuambukiza ya Marekani.

Katika ripoti iliyochapishwa na jarida la kitaalamu katika masuala ya afya la New England, watafiti walitoa dozi mbili za dawa katika majaribio kwa watu 45 waliojitolea, ambao umri wao ni kati ya miaka 18 mpaka 55.

Watafiti wanasema kwamba hakuna hata mmoja kati ya waliojitolea amepata madhara makubwa, lakini nusu yao walipata kwa kiwango kidogo ama cha kati hali ya kichwa kuuma, uchovu, homa, kubanwa na misuli na maumivu katika sehemu walizodungwa chanjo hiyo.

WAKAZI HONG KONG WAELEZA WASIWASI WAO CHINI YA SHERIA MPYA

Wakazi wa Hong Kong wanasema wanajikuta katika hali ya hofu toka kutungwa kwa sheria ya usalama wa taifa na China bara.

Licha ya hayo wachambuzi wanasema kwamba kutokana na wasiwasi huo kuchangia juhudi zao za kutaka uhuru, wataendelea kupambania kupata haki zao za kidemokrasia wanazodai.

Sheria iliyopitishwa na bunge la China hapo Juni 30, na kuanza kutumika Hong Kong Julai mosi, inatoa hukumu ya mpaka kifungo cha maisha gerezani kwa makosa ya nia ya kujitenga, ugaidi, kutotii mamlaka, na kula njama kwa mamlaka.

Toka kuanza kutekelezwa kwa sheria hiyo, matangazo ya waandamanaji yanayotaka uhuru ama yale yanayo kosoa serekali yameondoka kabisa katika mitaa ya Hong Kong.

Serekali inadai ujumbe wa maandamano wa “Ukombozi wa Hong Kong, mapinduzi ya wakati wetu” ni kinyume cha sheria chini ya sheria mpya, kwa kushutumu kwamba ujumbe huo unaodai uhuru upo katika vipengele vya kutaka kujitenga na kutotii mamlaka.

XS
SM
MD
LG