Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:07

Rais wa Mali amejiuzulu na kulivunja bunge la nchi hiyo


Rais wa Mali aliyejiuzulu Ibrahim Boubacar Keita. June 30, 2020.
Rais wa Mali aliyejiuzulu Ibrahim Boubacar Keita. June 30, 2020.

Katika hotuba fupi kupitia televisheni ya taifa Keita alisema “sitaki damu imwagike ili niendeleaa kuwa mamlakani”. Wanajeshi walioasi katika mji mkuu wa Mali walimkamata Keita na Waziri Mkuu, Boubou Cisse

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, amejiuzulu na kulivunja bunge saa chache tu baada ya maafisa wa jeshi kumkamata na kumzuilia pamoja na maafisa wa ngazi ya juu katika serikali yake. Katika hotuba fupi kupitia televisheni ya taifa Keita alisema “sitaki damu imwagike ili niendeleaa kuwa mamlakani”.

Mapema Jumanne wanajeshi walioasi katika mji mkuu wa Mali walimkamata Keita na Waziri Mkuu, Boubou Cisse na waliwaweka kizuizini. Ripota wa Idhaa ya Kifaransa ya Sauti ya Amerika anasema rais alikamatwa akiwa nyumbani kwake huko Bamako na alichukuliwa hadi kambi ya jeshi katika mji unaoitwa Kati uliopo kiasi cha kilomita 15. Waziri Mkuu Cisse naye alipelekwa kwenye kambi hiyo hiyo.

Milio ya risasi ilizuka kwenye mji uitwao Kati mwanzoni mwa siku. Ripota aliyeko Mali aliiambia VOA kwamba wanajeshi waliingia katika mapigano, walichukua bunduki na kuanza kufyatua risasi hewani, waliingia mtaani na kufunga njia kuelekea kwenye kambi hiyo.

Hakuna vifo vyovyote vilivyoripotiwa katika ghasia hizo. Uasi katika kambi hiyo hiyo ulichochea mapinduzi dhidi ya Rais wa Mali, Amadou Toumani Toure mwaka 2012.

XS
SM
MD
LG