Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:43

Jumuia ya kimataifa yapongeza usitishaji mapigano Libya


Mlibya akipeperusha benders ya taifa watu walipokua wanaherehekea mjini Tripoli capo June 4 2020, baada ya kufurushwa na wapiganaji wa upinzani.
Mlibya akipeperusha benders ya taifa watu walipokua wanaherehekea mjini Tripoli capo June 4 2020, baada ya kufurushwa na wapiganaji wa upinzani.

Umoja wa Ulaya, EU umnesema hii leo kwamba kuna matumaini mazuri kwa libya baada ya serikali mbili zinazo hasimiana nchini humo kutangaza usitishaji wa mapigano Ijumaa na kupanga kufanyika uchaguzi mkuu kote nchini.

Matukio hayo ambayo hayakutazamiwa yalitokea Ijuma, yanafuatia ziara kadhaa za wanadiplomasia wa juu kutoka nchi mbali mbali huko Tripoli katika wiki chache zilizopita na makubaliano na mikataba kadhaa iliyofikiwa bila kutekelezwa.

Baraza la Ushirikiano wa nchi za Ghuba GCC limepongeza pia tangazo hilo la kusitisha mapigano na kuzihimiza pande zote kuchukua hatua thabiti kuelekea muelewano wa kudumu.

Mkuu wa masuala ya kigeni wa EU, Josep Borrell, ameeleza matukio hayo kama “hatua ya kwanza thabiti kuendelea mbele.”

Amesema tangazo linaonisha dhamira ya viongozi wa libya kutaka kukamilisha mvutano na mzozo kati yao na kubuni matumaini mepya kwa faida ya wote kuelekea suluhisho la kudumu la amani na kisiasa.

Manadiplomasia huyo alihimiza kuwepo na hatua thabiti kuwezesha kuwepo na usitishaji wa kudumu wa mapigano na kuanzishwa upya utaratibu wa kisiasa.

Libya imekua katika hali ya ghasia na mapigano tangu kupinduliwa na kuuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Moammar Ghadafi 2011.

XS
SM
MD
LG