Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:08

Serikali ya Libya yasitisha mapigano


Nyumba zimeharibiwa kufuatia mapigano kati ya Serikali ya Libya na kikundi cha Islamic State katika mji wa Sirte, Libya Agosti 18, 2020.
Nyumba zimeharibiwa kufuatia mapigano kati ya Serikali ya Libya na kikundi cha Islamic State katika mji wa Sirte, Libya Agosti 18, 2020.

Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa Ijumaa imetangaza sitisho la mapigano. Serikali hiyo yenye makao makuu mjini Tripoli, inadhibiti eneo la magharibi mwa Libya.

Serikali hiyo inapambana na waasi wa mashariki mwa Libya ambao wanaongozwa na Jenerali Halifa Haftar. Wanajeshi wa Haftar walifanya mashambulizi kwa zaidi ya mwaka moja ili kuuteka mji mkuu Tripoli, kabla ya kurejeshwa nyuma hapo mwezi juni na jeshi la Uturuki, linaloliunga mkono jeshi la serikali ya Tripoli, GNA.

Mkuu wa serikali ya GNA Fayez al Sarraj ametoa agizo kwa wanajeshi wote kusitisha mara moja mapigano na operesheni za kijeshi katika maeneo yote ya Libya, taarifa ya serikali imesema.

Jenerali Haftar na jeshi lake la LNA, walikuwa hawajatoa taarifa yoyote kuhusu uamuzi huo wa serikali ya GNA, licha ya kuwa kiongozi wa bunge lenye makao yake mashariki mwa Libya ambaye ni mshirika wa Haftar, ametoa taarifa akiomba mapigano yasitishwe nchini kote.

Jeshi la LNA la jenerali Haftar linaungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Russia.

XS
SM
MD
LG