Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yameishutumu Ufaransa mara kwa mara kwa kuendelea kutoa silaha kwa mataifa ya Ghuba, licha ya kuwepo madai ya uhalifu wa vita na vifo vya raia wakati wa operesheni za kijeshi nchini Yemen.
Akizungumza na waandishi wa habari alipowasili Romania kwa mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, Macron amesema kwamba silaha zake hazitumiki dhidi ya raia, bali katika vita dhidi ya ugaidi.
Kulingana na mashirika ya kutoa misaada, vita vya Yemen, ambavyo vimedumu kwa muda wa zaidi ya miaka minne, vimeua maelfu ya watu, idadi kubwa wakiwa ni raia.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.