Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:14

India, Saudi Arabia kusaini mikataba ya miundombinu, nishati


Prince Mohammed bin Salman na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi at Hyderabad House, New Delhi, India, Feb. 20, 2019.
Prince Mohammed bin Salman na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi at Hyderabad House, New Delhi, India, Feb. 20, 2019.

Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia Mohammad Bin Salman Al Saud, ameanza ziara yake nchini India inayoghubikwa na shambulizi la Kashmir lililouwa polisi wa kijeshi 40.

Mtoto wa mfalme amesema kwamba ziara yake inakusudia kujenga uhusiano mwema wa kihistoria kati ya India na Saudi Arabia kwa ajili ya watu wa nchi hizo zote mbili.

Prince Mohammad anatarajiwa kusaini mikataba ya miradi mbalimbali ikiwemo miundombinu na nishati nchini India, wakati utawala wake ukiwa umechafuliwa kimataifa, kufuatia mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa makala wa gazeti la Washington Post la Marekani, Jamal Khashoggi.

Bin Salman amelakiwa kwa sherehe nje ya makao ya rais katika mji mkuu wa New Delhi.

Ziara hiyo ilyoanza siku chache baada ya shambulizi la Kashmir ambalo kundi la wapiganaji la Jaish – e- Mohammad, lenye makao yake Pakistan, lilidai kuhusika.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

DC

XS
SM
MD
LG