“Hatua kubwa imefikiwa, “ Trump amesema ya kuboreshwa kushirikiana majukumu kati ya wanachama wa mataifa huru 29 waliosaini mkataba wa NATO, lakini alisema kuwa Ujerumani, ukweli, haichangii kiwango kinachostahiki.
Trump amesisitiza wasiwasi wake kuwa wakati Marekani inatumia fedha nyingi kuilinda Ulaya, “wao wanatunyonya sisi katika biashara.”
Trump, akiwa pamoja na Jens Stoltenberg mbele ya Ofisi ya Ikulu ya Oval, amempongeza kiongozi huyo kwa uhadori wake wa kuiongoza NATO.
“Sisi tunashirikiana vizuri kabisa,” Trump amesema akimsifia waziri mkuu huyo wa zamani wa Norway.
Rais alijisifia juu ya mchango wake katika kubadilika kwa umoja huo wa NATO ambao siku za nyuma alisema kuwa ulikuwa umepitwa na wakati.
“Kama mnavyojua wakati nachukuwa madaraka umoja huo ulikuwa hauko vizuri, hivi sasa wanapiga hatua” kwa wanachama wake kufikia lengo la kuchangia asilimia mbili ya pato lao la kitaifa (GDP) katika ulinzi.
“Lakini nafikiri lazima iwe zaidi ya kiwango hicho,” ameongeza Trump.
Stoltenberg amemshukuru rais kwa uongozi wake shupavu katika kushirikiana kwenye majukumu,” akiongeza, “sisi tumechukuwa hatua za pamoja kukabiliana na ugaidi na tunawekeza zaidi katika hilo.”
Trump aliulizwa na mwandishi kuhusu Russia, hasimu wa Vita Baridi ambayo ilipelekea kuundwa kwa umoja huo.
“Natumai kuwa haitaendelea kuwa ni tishio la usalama. Nafikiri tutaweza kushirikiana na Russia,” amejibu Trump, ambaye kampeni ya uchaguzi wake 2016 ulikuwa umemurikwa na uchunguzi wa miaka miwili uliofanywa na mchunguzi maalum juu ya madai ya kuwa na mafungamano na Moscow.
Katika mikutano ya baadae iliyofanyika katika Chumba cha Baraza la Mawaziri, Stoltenberg, akiwa upande wa pili mkabala na Trump, alisema Russia imekuwa ikikiuka mkataba wa Silaha za Masafa ya Kati za Nyuklia (INF), akieleza kuwa “Washirika wa NATO wamekuwa wakiunga mkono kikamilifu msimamo wa Marekani juu ya hilo .”