Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:16

Kampeni ya Russia ya 'Habari Feki' Inadhamiria Kuihujumu NATO


Wanajeshi wa Ujerumani wakiwa Lithuania
Wanajeshi wa Ujerumani wakiwa Lithuania

Barua pepe zikiwashutumu askari wa Ujerumani ambao wako Lithuania kwamba wamefanya vitendo vya ubakaji, zilizotumwa wiki hii kwa vyombo vya habari vya nchi hiyo, zilikuwa zinakusudia kulichafua jeshi la NATO.

Wachambuzi wa mambo ya kijeshi katika NATO wanasema kuwa hiyo ni kampeni ya Russia kupitia “habari feki” zenye kusudio la kufanya umma upoteze imani ya umoja huo wa kijeshi.

Barua pepe hizo ambazo zilitumwa kwa vyombo vya habari kadhaa vya Lithuania Februari 14, vimedai kuwa askari wa Ujerumani ambao wako katika jimbo la Baltic waliwabaka watoto wakike huko Lithuania.

Baadhi ya vyombo ya habari vya Lithuania viliripoti madai hayo, ambayo yalikanushwa na jeshi la polisi la Lithuania, ambao waliendelea kufuatilia chanzo cha anwani hizo za itifaki ya internet ambazo zilihusika kusambaza madai hayo.

“Lile tunalojua, polisi wa Lithuania baada ya kufanya uchunguzi wamefikia hitimisho kuwa hakuna malalamiko kutoka upande wa watoto hao wala hakuna mtu yoyote aliyeshuhudia na wala hakuna mtu aliyetajwa kuhusika,” amesema msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani.

Taarifa za tukio hili lenye kupotosha linafanana na kile kinachojulikana kama kesi ya Lisa mwaka jana, ambapo vyombo vya habari vya Russia mara ya kwanza viliripoti na baadae kusababisha mtafaruki Ujerumani.

Kesi hiyo ilikuwa inahusu madai yaliofanywa na mtoto wa miaka 13 mwenye asili ya mataifa mawili, Russia na Ujerumani, kuwa alikuwa ametekwa na kubakwa na mhamiaji wa Kiarabu mjini Berlin.

Lakini ilikuja kujulikana kwamba msichana huyo hakutekwa lakini alikuwa ametunga habari hiyo, akitaka kuficha wazazi wake kwamba amekwenda kustarehe na kipenzi chake usiku huo nyumbani kwake. Kesi ya Lisa iliongeza mvutano uliokuwepo katika mahusiano kati Berlin na Moscow.

XS
SM
MD
LG