Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:13

Marekani inaelekea katika mgongano na EU


Rais Donald Trump (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo
Rais Donald Trump (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo

Uamuzi wa Rais Donald Trump kujiondoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran imeifanya Marekani kuwa na mgongano na baadhi ya washirika wake wa karibu Umoja wa Ulaya (EU).

Trump ameamrisha kuwekwa vikwazo kamili dhidi ya makampuni ambayo yanaendelea kufanya biashara na Iran, hatua iliyo sababisha wasiwasi, hasa nchini Ufaransa na Ujerumani, ambako makampuni kama vile Airbus na Volkswagen yamesaini mikataba ya mamilioni ya dola na Tehran.

Masaa kadhaa baada ya kuapishwa, Waziri wa Mambo ya Nje mpya Mike Pompeo alisafiri kuelekea Makao Makuu ya Umoja wa kujihami wa Ulaya (NATO) huko Brussels ambako aliainisha kwa kiwango gani Marekani inathamini mahusiano ya pande mbili za bahari ya Atlantic kama ni nguzo ya usalama na utulivu wa dunia.

Lakini uhusiano huo umepatwa na misukosuko hivi karibuni, ambapo Marekani imekuwa ikisema kuwa itaweka vikwazo dhidi ya kampuni yoyote inayofanya biashara na Iran.

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel alizungumza Jumanne juu ya uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump wiki iliyopita kujiondoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran.

Merkel amesema: “Hivi sasa tumeona mabadiliko makubwa ya mahusiano kati ya Ujerumani na Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani, wakati ambapo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinamaoni kuwa mkataba dhidi ya silaha za nyuklia za Iran ni mkataba ambao unamapungufu lakini ni lazima tuheshimu mkataba huo.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Javad Zarif amekutana na mwenzake wa Umoja wa Ulaya huko Brussels Jumanne kujadili jinsi ya kuuendeleza mkataba huo wa nyuklia wa Iran.

Zarif amesema :” Kwa hiyo, ni juu ya Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa Umoja huo kuhakikisha maslahi yao na maslahi yetu yanalindwa na kuwa uvunjifu wa mkataba huo uliofanywa na Marekani usiendekezwe.”

Waziri Pompeo amesema kuwa mkataba wa nyuklia umetengeneza fursa ya utajiri nchini Iran ambao unaendeleza “harakati hatarishi,” na kuwa kujiondoa kwa Marekani kusudio siyo dhidi ya Umoja wa Ulaya. Lakini wataalamu wanasema kuwa watu wa Ulaya wamekasirishwa na Marekani kwa kuweka upya vikwazo, na wanahisi hawana nafasi kubwa ya kuchagua wanachokitaka.

XS
SM
MD
LG