Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:00

Trump asifia madai yake kwa NATO yamezaa matunda


Rais Donald Trump amesema ameweza kupata ahadi za wanachama wa NATO katika kuongeza bajeti zao za ulinzi baada ya masiku kadhaa ya kiongozi huyo wa Marekani kulalamika kuwa Washington ilikuwa inabeba mzigo mkubwa katika kuwasaidia washiriki wake.

“Wamekubali kwa kiwango kikubwa kuongeza majukumu yao na hivi sasa tunayo furaha na NATO iliyokuwa na nguvu, sana, sana kabisa ,” Trump aliwaambia waandishi wakati wa kufunga mkutano wa washiriki huko Brussels. Lakini hakueleza nchi gani iliahidi kitu gani.

“Baadhi wanachangia asilimia 2 ya (Pato la Taifa), wengine wamekubali kwa moyo mkunjufu kuongeza kiwango kufikia asilimia 2,” amesema. Siku moja kabla, Trump alipendekeza kuwa washiriki wa NATO waweke ahadi ya kutumia asilimia 4 ya Pato la Taifa katika ulinzi ifikapo 2024.

“Naimani na NATO,” Trump amesema Alhamisi, lakini aliongeza kuwa Marekani imekuwa haitendewi haki kwa kutoa huduma ya zaidi ya miongo saba katika ushirika huo, akidai kuwa Washington ilikuwa inabeba mzigo wa asilimia 70 -90 katika kuisaidia NATO, ambapo amesema sio haki kwa walipa kodi wa Marekani.

Trump alisema anaweza kuiondoa Marekani kutoka NATO bila ya kupata idhini ya Bunge la Marekani, lakini akasema “hilo sio muhimu” baada ya ahadi iliyotolewa na wanachama wa ushirika huo. “Kulikuwa na moyo wa mshikamano mkubwa katika chumba hicho… kukubaliana kwa nguvu kubwa.”

Viongozi wa NATO walikuwa wanatarajia Alhamisi kutekeleza zaidi ya kile anachokidai Rais Trump cha kuongeza matumizi ya ulinzi, na kujikita katika kumaliza vita ya muda mrefu huko Afghanistan.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg anataka viongozi wakubaliane kufadhili majeshi ya usalama ya Afghan mpaka 2014, pamoja na watu nchi za magharibi kuwa wamechoshwa na nchi zao kujihusisha na mgogoro huo.

XS
SM
MD
LG