Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:47

Trump awalaumu viongozi wa NATO


Rais Donald Trump akiwa Makao Makuu ya NATO
Rais Donald Trump akiwa Makao Makuu ya NATO

Rais Donald Trump amewaambia viongozi wa NATO kuwa wanachangia kile anachokiona ni fedha kidogo katika ulinzi, na kutaka washirika hao kuangalia zaidi masuala ya ugaidi.

“NATO ya siku za usoni lazima iwe na mtizamo mkubwa zaidia juu ya ugaidi na uhamiaji na pia vitisho vya Russia na mpaka wa NATO upande wa mashariki and kusini.

Haya masuali ya ulinzi yanaleta wasiwasi na sababu zilezile ambazo nimekuwa nikizieleza waziwazi na Waziri Stolteberg na wanachama wengine wa umoja kwa kusema kuwa wanachama NATO ni lazima wachangie kiwango chao halisi na kufikia majukumu ya kifedha.” Trump aliwaambia viongozi wa NATO huko Brussels.

Amesema kati ya wanachama 23 ya wale 28 hawalipi kiwango wanachostahili kulipa, kitu ambacho hatuwafanyii haki wananchi wa Marekani.

Trump pia anasema shambulizi la bomu la Manchester hivi karibuni “linaonyesha ukubwa wa uovu wa ugaidi uanotukabili.”

Mapema Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema ataeleza masikitiko yake kwa Trump juu ya kuvuja kwa habari Marekani kwa vyombo vya habari zilizoeleza kwa undani uchunguzi wa shambulizi la bomu la Manchester.

May amewaambia waandishi kuwa ushirikiano wa kina wa ulinzi na usalama kati ya Marekani na Uingereza “umejengwa katika dhana ya kuaminiana na sehemu ya hilo ni kujua kuwa tunaweza kubadilishana taarifa za kiusalama kwa kuaminiana.”

“Nitaliweka wazi jambo hili kwa Rais Trump leo kuwa taarifa za kiusalama zinabadilishwa tu na vyombo vya usalama na ni lazima ziwe salama,” amesema Waziri Mkuu.

Katika tamko lililotolewa na ikulu ya White House, Trump amesema kuwa “ "Madai ya kuvuja kwa taarifa hizo zilizotolewa na vyombo vya serikali ni za kusikitisha sana,” na naongeza “ Nataka Idara ya Sheria na vyombo vingine husika kuliangalia kwa ukamilifu tatizo hili, na ikiwa inastahili basi waliofanya kosa hili washtakiwe kwa kufuata hatua zote za kisheria.

XS
SM
MD
LG