Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:39

Tanzania : Upinzani wapinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa


Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHAUMA Hashim Rungwe
Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHAUMA Hashim Rungwe

Vyama vya Siasa 15 nchini Tanzania vimesema vinapinga na vinataka mabadiliko ya Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Vyama vya siasa uliosomwa bungeni Novemba 16, 2018.

Vyama hivyo vimedai kuwa muswada huo una vipengele vingi vinavyo kandamiza vyama hivyo na kuwataka wabunge na wadau wa siasa kuupinga.

Akiwasilisha tamko hilo kwa niaba ya wenzake mbele ya waandishi wa habari Jumapili jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Hashim Rungwe amesema sababu kuu ya kupinga muswada huo ni kwenda kinyume na katiba ambayo imetoa uhuru kwa wanasiasa kujumuika na kufanya kazi zao pamoja lakini sheria hiyo mpya imezuia.

Gazeti la Mtanzania limeripoti mwanasiasa huyo amesema kuwa zuio la wanasiasa kutokufanya mikutano ya hadhara na kunadi sera zao kwa wananchi ni kinyume na sheria ya nchi kwani hata Katiba inatambua uwepo wa vyama vingi vya siasa nchini hivyo kuwazuia ni kwenda kinyume na katiba.

“Muswada huu si rafiki kwetu na tumetumia siku ya Uhuru wa nchi kudai uhuru wa vyama vya siasa ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu hivyo hatutakubali uhodhiwe au kupokonywa na mtu.
“Tunatoa wito kwa Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa kupinga sheria hizi kandamizi, ” amesema.

Aidha vyama vilivyo ungana na kutoa tamko la kupinga muswada huo Ni Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Democratic Party ( DP), Chama cha NCCR MAGEUZI, Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), National League for Democracy (NLD), Chama cha United People’s Democratic Party (UPDP) na Chama cha Kijamii (CCK).

XS
SM
MD
LG