Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:37

Chadema yasusia uchaguzi baada ya mawakala, mgombea kupigwa


Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jumapili kimetangaza kujitoa katika uchaguzi mdogo kata ya Songoro wilayani Arumeru, Arusha, Tanzania, kutokana na vurugu na mwanachama wao kushambuliwa kwa kisu.

Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema baada ya mashauriano kati ya chama na mgombea, Godluck Nanyaro wameona hakuna sababu ya kuendelea na uchaguzi.

“Tumeamua kuwaondoa vituoni mawakala wetu katika vituo 14 kutokana na kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu,” amesema.

Gazeti la Mtanzania limeandika kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhan Ng’anzi, amethibitisha kutokea kwa vurugu na kukanusha kuwa hakuna mgombea aliyechomwa kisu katika Kata ya Kaloleni.

“Kilichotokea ni kwamba mgombea wa kata hiyo ameshambuliwa na watu wasiojulikana na sasa hivi tumefungua kesi ili kuanza uchunguzi," amesema.

Lakini Kamanda amesema kuwa aliyechomwa kisu ni mwanachama wa CCM na tukio hilo limetokea eneo la Mianzini.

"Baada ya kukutana na kundi jingine ukatokea mzozo baina ya makundi hayo mawili ambapo mtu mmoja kati ya makundi hayo akachomoa kisu akamchoma na aliyefanya hivyo tunamshiklilia hapa kituoni kwa mahojiano zaidi. Kwa ujumla uchaguzi katika mkoa wetu unaendelea vizuri, usalama upo wa kutosha," ameeleza Kamanda.

Chadema inadai kuwa inajitoa kutokana na mgombea wake na mawakala wake kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

XS
SM
MD
LG