Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 05:09

Sababu tano zilizomfanya Mtatiro kuihama CUF Tanzania


Julius Mtatiro wa CUF
Julius Mtatiro wa CUF

Naibu Katibu Mkuu wa zamani na mmoja kati ya wanachama mashuhuri zaidi wa Chama wa Wananchi, CUF, nchini Tanzania, Julius Mtatiro, alitangaza siku ya Jumamosi kwamba amejitoa katika chama hicho.

Mtatiro alichukua uamuzi huo akiwa katika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya chama hicho chini ya Maalim Seif Sharif Hamad.

Wakati anatangaza uamuzi huo, alitaja sababu tano zilizomsukuma kufanya uamuzi huo.

Alisema kuwa sababu ya kwanza ni kutoridhishwa na hali ya ushiriki na mchango wake kwenye siasa za CUF.

Ya pili ni mgogoro wa kiuongozi unaoendelea kukikumba chama hicho. Na jambo la tatu ni kutoridhishwana ushiriki wake kama kijana na kiongozi katika kuchochea maendeleo ya nchi.

Jambo la nne ni ajenda ya maendeleo ya nchi na la tano ni mustakbali wake kuhusu masuala ya siasa.

Mtatiro alitangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kueleza kuwa ameanza kwa kuzungumza na waandishi wa habari na kutangaza azma yake ambayo ameitafakari kwa muda mrefu kabla ya kuwataarifu viongozi wa CCM ambao amewaomba wampokee.

“Nawaambia Watanzania kwamba kuanzia leo nitaanza kufanya siasa za maendeleo ili kumsaidia Rais John Pombe Magufuli," alisema Mtatiro.

Pia amesema kuanzia Jumamosi atajikita katika kushiriki kufanya siasa za maendeleo na hasa kuunga mkono jitihada za Rais.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa juhudi za Magufuli za kuleta maendeleo zimesababisha Mtatiro kuamua kubadili mawazo na kuingia CCM.

XS
SM
MD
LG