Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:19

Somalia : Mahakama ya kijeshi yawahukumu kifo wanajeshi wawili wa Uganda


Wanawake Somalia wakipinga vitendo vya tume ya kulinda amani Somalia (AMISOM) nje ya Hospitali ya Erdogan kufuatia mauaji ya raia wakati wa mapambano kati ya wanajeshi wa Amisom na wapiganaji wa al Shabaab katika mkoa wa Lower Shabelle, Mogadishu, Somalia. REUTERS/Feisal Omar
Wanawake Somalia wakipinga vitendo vya tume ya kulinda amani Somalia (AMISOM) nje ya Hospitali ya Erdogan kufuatia mauaji ya raia wakati wa mapambano kati ya wanajeshi wa Amisom na wapiganaji wa al Shabaab katika mkoa wa Lower Shabelle, Mogadishu, Somalia. REUTERS/Feisal Omar

Wanajeshi wawili wa Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) wanaohudumu kwenye tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) wamehukumiwa kifo na wengine watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 39 jela kutokana na vifo vya raia. 

Mahakama ya Kijeshi ya Uganda iliendesha kesi mjini Mogadishu na imewakuta maafisa wawili hao na makosa ya kuua raia kwa makusudi karibu na ujirani wa Golweyne ilioko sehemu ya mkoa wa Lower Shabelle nchini Somalia Agosti mwaka 2021, na wengine watatu walihukumiwa kifungo cha jela kwa kushiriki katika uhalifu huo,” Waziri wa Sheria wa Somalia, Abdulkadir Mohamed Nur, ameiambia VOA Idhaa ya kisomali Jumamosi.

Hukumu hii itakuwa fundisho kwa tume ya AMISOM kwamba hakuna atakaye weza kukimbia iwapo ataua raia wa Somalia,” Nur amesema.

Tukio hilo lilitokea Agosti 10, wakati wanajeshi wa Uganda waliokuwa katika doria kwenye njia kuu ya usafirishaji kati ya vijiji vya Beldamin na Golweyn walipowafyatulia risasi raia katika eneo la shamba kiasi cha kilomita 120 kusini magharibi mwa Mogadishu, kulingana na maafisa wa eneo na taarifa ya Amisom.

Ndugu na mashuhuda wawalishutumu wanajeshi wa AMISOM kwa kuweka miili ya baadhi ya waathirika hao katika machimbo yanayolindwa ya mbali kabla ya kulipuliwa, ikizua hasira za wenyeji katika eneo na maandamano mjini Mogadishu.

Wakati huo, AMISOM iliripoti kuwa wanajeshi wake walikuwa wanapambana na shambulizi la al-Shabaab.

Jeshi la AMISOM lilikiri mwezi uliopita, hata hivyo, kuwa walinzi wake wa amani kinyume cha sheria waliwaua raia saba katika mapambano ya bunduki kati ya wanajeshi wa kikosi cha kulinda amani na wapiganaji wa al-Shabaab wenye uhusiano na al-Qaida, wakiahidi kuwa wanajeshi waliohusika watawajibishwa.

Kesi hiyo imekuwa ikisikilizwa mahakamani tangu Octoba 5 katika kambi yenye ulinzi mkali ya Halane karibu na uwanja mkuu wa ndege Mogadishu, ambako makao makuu ya UN na Amisom yapo.

Baadhi ya ndugu wa waathirika hao na wawakilishi wa wakulima wa eneo la Lower Shabelle walihudhuria kesi hiyo, na walikuwepo mahakamani wakati hukumu hizo zikitolewa.

Msemaji wa ndugu hao wa marehemu, Hussein Osman Wasuge akizungumza na vyombo vya habari vya Somalia walikuwa wameridhishwa na hukumu iiyofikiwa.

“Ingawaje kulikuwa hakuna mawakili kutuwakilisha, mmoja kati yetu na wanajeshi sita wa Uganda waliruhusiwa kutoa ushahidi dhidi ya askari wanaotuhumiwa kwa siku mbili,” amesema Wasuge. “Tumefurahi sana na uamuzi wa mahakama na tunatarajia fidia itatolewa kwa familia za wale waliouawa.

Wanajeshi wa Uganda walikuwa katika mji mkuu, Mogadishu, na mkoa wa Lower Shabelle, ambapo wanakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara na uvamizi wa wapiganaji wa kikundi cha al-Shabab.

XS
SM
MD
LG