Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:52

Umoja wa Afrika kuongeza operesheni za kijeshi dhidi ya makundi ya kiislam


Viongozi wa Umoja wa Afrika katika ufunguzi wa mkutano wa 30 huko Addis Ababa Ethiopia.
Viongozi wa Umoja wa Afrika katika ufunguzi wa mkutano wa 30 huko Addis Ababa Ethiopia.

Umoja wa Afrika unasema utaongeza na kupanua operesheni zake za kijeshi za kupambana na makundi ya Kiislam yenye mahusiano na Al-Qaeda

Umoja wa Afrika unasema utaongeza na kupanua operesheni zake za kijeshi za kupambana na makundi ya Kiislam yenye mahusiano na Al-Qaeda nchini Somalia na kujumuisha nchi zingine wanachama, wakati muda wake wa hivi sasa unakaribia kumalizika ifikapo Desemba 31.

Taifa hilo la Pembe ya Afrika limekabiliwa na ukosefu wa utulivu tena katika miezi ya hivi karibuni, na ucheleweshaji wa uchaguzi uliodumu kwa muda mrefu na mvutano unaoendelea kati ya rais wake na waziri mkuu ikiondoa lengo lake kutoka kwenye kupambana na uasi unaofanywa na wapiganaji wa Al-Shabaab.

Licha ya kufukuzwa kwa wanamgambo hao kutoka Mogadishu muongo mmoja uliopita, serikali ya Somalia inadhibiti sehemu ndogo tu ya nchi hiyo, kwa msaada muhimu wa wanajeshi 20,000 kutoka Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, Amisom.

AMISOM Jumapili jioni ilisema Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika limekubali kubadili malengo yake na kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa mataifa ambayo itawawezesha nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika wenye nia ya kujiunga na operesheni dhidi ya wanamgambo hao wa Kiislam.

XS
SM
MD
LG