Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:38

ICJ kutoa uamuzi kuhusu mzozo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia


Nembo ya mzani wa sheria
Nembo ya mzani wa sheria

Uamuzi unaweza kueleza ni nani anayo haki ya kutumia mafuta na gesi katika maji ya kina kando ya pwani ya Afrika mashariki. Somalia iliwasilisha kesi hiyo mwaka 2014 katika mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na mizozo ya mipaka kati ya majimbo

Mahakama ya Sheria ya Kimataifa (ICJ) Jumanne inatoa uamuzi wake kuhusiana na kesi iliyowasilishwa na Somalia dhidi ya Kenya juu ya mpaka wa sehemu zinazogombaniwa za bahari ya Hindi zinazoaminika kuwa na utajiri wa mafuta pamoja na gesi.

Uamuzi huo unatolewa wiki moja baada ya Nairobi kusema kuwa imebatilisha kutambuliwa kwa mamlaka ya mahakama. Somalia iliwasilisha kesi hiyo mwaka 2014 katika mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na mizozo ya mipaka kati ya majimbo.

Uamuzi unaweza kueleza ni nani anayo haki ya kutumia mafuta na gesi katika maji ya kina kando ya pwani ya Afrika mashariki. Kesi katika ICJ ambayo pia inajulikana kama mahakama ya dunia inatokana na mzozo wa mpaka wa baharini ambao ni zaidi ya kilomita za mraba laki moja (takribani maili 40,000 za mraba) zinazodaiwa na nchi zote mbili.

Mwezi Machi nchi ya Kenya ilisusia vikao vya hadhara huko The Hague.

XS
SM
MD
LG