Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 22:32

Uchaguzi wa wabunge unafanyika Somalia


Wabunge wa Somalia
Wabunge wa Somalia

Upigaji kura nchini Somalia unafanyika ili kuwachagua wabunge wa baraza kuu la bunge, ikiwa ni mchakato kuelekea uchaguzi wa urais ambao umecheleweshwa kutokana na hali ya kutoelewana ambayo imekuwa ikiandamana na vurugu.

Tayari wabunge wawili katika bunge lenye viti 275 wamechaguliwa katika shughuli iliyofanyika mjini Mogadishu chini ya uangalizi mkubwa wa maafisa wa usalama.

Somalia haijawahi kuandaa uchaguzi wa kitaifa wa mtu mmoja kura moja kwa mda wa miaka 50 sasa.

Uchaguzi unafanyika kwa kufuata mfumo uliotumiwa katika uchaguzi zilizopita, ambapo waakilishi 30,000 wa uko wanachagua wabunge 275 wabaraza kuu la bunge. Wabunge wanaochaguliwa huchagua maseneta 54.

Baada ya wabunge na maseneta kuchaguliwa, huapishwa na baadaye kuchagua rais.

XS
SM
MD
LG