Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:31

Viongozi Somalia wawasihi Rais na Waziri Mkuu kutafuta suluhu


Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, kushoto, na Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble, Mogadishu, Somalia, on Mei 27, 2021.
Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, kushoto, na Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble, Mogadishu, Somalia, on Mei 27, 2021.

Viongozi wa majimbo huko Somalia Ijumaa walitoa wito kwa Rais na Waziri Mkuu kumaliza ugomvi wao wakionya juu ya hatari ya kutokuwa na utulivu wa kisiasa katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.

Mzozo huo uliongezeka kwa haraka Alhamisi, wakati Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, ambaye ni maarufu kama Farmajo, aliposimamisha mamlaka ya utendaji ya Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble.

Kitendo hicho kilipingwa mara moja na Waziri Mkuu na kueleza kwamba kinakwenda kinyume na sheria.

Viongozi hao wawili wamekuwa wakivutana juu ya uteuzi wa maafisa wa juu wa usalama katika mzozo ambao unatishia kuhatarisha uchaguzi uliocheleweshwa mara kwa mara, na kuvuruga juhudi za kukabiliana na uasi wa Kiislam uliokuwepo kwa muda mrefu.

Viongozi wa majimbo matano huru ya Somalia waliwataka wahusika kuacha kutupiana maneno, na kutatua tofauti zao kupitia mazungumzo ya upatanishi na kuheshimu katiba ya mpito.

XS
SM
MD
LG