Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:37

Ripoti ya uchunguzi wa Russia kuingilia kati uchaguzi Marekani yatolewa rasmi


William Barr
William Barr

Moja ya habari zilizochukuwa uzito wa juu katika miaka miwili ya urais wa Donald Trump, Alhamisi imeingia katika hatua mpya.

Hatua hiyo ni kutolewa kwa taarifa ya uchunguzi alioufanya Mwendesha Mashtaka Maalum Robert Mueller juu ya hujuma ya uchaguzi na madai ya Trump kuzuia sheria kuchukua mkondo wake.

Mwanasheria Mkuu William Barr, katika mkutano wake na waandishi wa habari Alhamisi amesema kuwa ripoti ya Mwendesha mashtaka maalum inaondoa dhana yoyote ile ya tuhuma dhidi ya Rais Trump juu ya kushirikiana kwake na Moscow na baada ya kuchukuwa madaraka Trump alikuwa hana “nia yoyote ya ufisadi” ya kuzuia sheria kuchukuwa mkondo wake.

Bunge la Marekani na wananchi wa Marekani kwa mara ya kwanza wamepata fursa ya kuona maelezo ya ripoti hiyo kwa kile ambacho Mueller alikuwa anakifanyia uchunguzi, wakati yeye na timu yake ya wachunguzi wa serikali kuu walipokuwa wanatafuta kujua iwapo kampeni ya Trump au washiriki wake walishirikiana na Russia katika juhudi zake za kuingilia kati uchaguzi wa mwaka 2016, ambao ulimpa ushindi Trump.

Idara za upelelezi za Marekani mwanzoni mwa mwaka 2017 walifanya tathmini juu ya Russia, wakielekeza uchunguzi wao kwa Rais Vladimir Putin, kuwa aliamuru kampeni ifanyike kuvuruga uchaguzi na alikuwa anakusudia kwamba Trump ashinde.

Watu ambao wanaifahamu ripoti hiyo ya Mueller ya kurasa 400 ambao waliongea na Magazeti ya Washington Post na The New York Times wamesema waraka uliotolewa Alhamisi utakuwa umepunguzwa kidogo na utatoa maelezo ya kina juu ya tuhuma mbalimbali dhidi ya Trump juu ya kuzuia uchunguzi wa serikali kuu kuhusiana na Russia kuingilia kati shughuli mbalimbali za uchaguzi.

Wakati huohuo Barr ametoa barua fupi yenye muhtasari wake juu ya mambo aliyoyabaini Mueller, na lililochukua uzito ni kuwa kampeni ya Trump haikushirikiana na Russia na kwa maoni ya Barr taarifa ya uchunguzi wa Mueller hauna ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai kwamba rais alizuia sheria kufuata mkondo wake.

XS
SM
MD
LG