Uchunguzi huu ni moja ya habari kubwa zilizoghubika vyombo vya habari katika miaka miwili ya urais wa Donald Trump.
Ripoti hiyo ambayo baadhi ya vipengere vinavyo husiana na usalama wa taifa vitafunikwa kwa wino mweusi wakati ikikabidhiwa kwa Baraza la Wawakilishi.
Mwanasheria Mkuu William Barr anatarajiwa kutoa ripoti Alhamisi kwa umma mubashara kupitia vyombo vya habari na kutoeleza baadhi ya masuala ambayo ni nyeti kwa usalama wa taifa.
Baadae Mueller atatuma nakala ya ripoti hiyo kwenye Baraza la Wawakilishi na itawekwa pia katika mtandao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Baraza la Wawakilishi, Mdemokrat Jerrold Nadler amesema mambo “yanajieleza yenyewe mwanasheria mkuu alichukua hatua za kufupisha taarifa hiyo na kuchagua mambo anayotaka katika barua yake aliyotuma kwenye bunge la Marekani Machi 24."
Aliongeza kusema kuwa : "Pili alizuia baadhi ya mambo yalioandikwa na mwendesha mashtaka maalum yaliotakiwa kuwasilishwa mbele ya umma."
Pia amedai kuwa jambo la tatu aliiambia White House juu ya ripoti hiyo kabla ya kupeleka nakala bungeni jambo liliowasaidia kuandaa majibu kwa ajili ya rais.”
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.