Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:54

Trump abeza uteuzi wa mchunguzi maalum


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump amebeza uteuzi wa mwanasheria maalum kuchunguza kampeni yake inayohusishwa na udukuzi wa Russia.

Uchunguzi huo unafungamana na uchaguzi wa rais mwaka jana, Trump akisema hatua hiyo ni “tukio la namna ya kipekee katika kumtafuta mchawi lililoelekezwa kwa mwanasiasa katika historia ya Marekani!”

Trump alikuwa ametatizika Jumanne baada ya kuteuliwa Robert Mueller, aliyekuwa mkurugenzi wa FBI, kuongoza uchunguzi ili ifahamike iwapo kati ya wasaidizi wa Trump yupo aliovunja sheria kwa kushirikiana na maafisa wa Russia katika juhudi za kumsaidia Trump kupata nafasi ya ushindi katika uchaguzi wa urais mwaka jana.

Katika maoni yake mapema asubuhi katika akaunti ya Twitter, Trump amelalamika kuwa mchunguzi maalum hajawahi kutajwa kuchunguza “vitendo vyote vya uvunjaji sheria vilivyotokea” katika kampeni ya uchaguzi wa mpinzani wake wa Chama cha Demokratik, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton, na uongozi wa aliyemtangulia wa Rais mstaafu Barack Obama.

Rais amesema pamoja na vitendo vyote vilivyokuwa kinyume cha sheria vilivyotokea katika kampeni ya Clinton na Uongozi wa Obama, hakukuwa na mwanasheria maalum aliyeteuliwa kuchunguza!

Jumuiya ya Usalama ya Marekani imehitimisha kuwa Moscow iliingilia kati kuvuruga uchaguzi kwa kumsaidia Trump kuchukua White House kwa kufanya udukuzi katika kompyuta za mkuu wa kampeni ya Clinton, John Podesta.

XS
SM
MD
LG