Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:22

Raia wa Russia 13 wafunguliwa mashtaka Marekani


Robert Mueller
Robert Mueller

Ofisi ya mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller imesema kuwa baraza la mahakama limewafungulia mashtaka raia wa Russia 13 na taasisi tatu za Russia Ijumaa

Pia ofisi yake imetoa vielelezo kamili juu ya mpango wao wa kuingilia kati uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwaka 2016, waendesha mashtaka wa serikali kuu wametangaza Ijumaa.

Mashtaka hayo yalioletwa na ofisi ya mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller, yanadai kuwa Russia iliweka taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii na matangazo yalionunuliwa kwa udanganyifu kwa kutumia jina la Wamarekani.

Mueller amesema kuwa hilo lilifanyika ili kupotosha maoni ya kisiasa wakati wa kinyang’anyiro cha urais kati ya Donald Trump wa chama cha Republikan na Hillary Clinton mpinzani wake wa Chama cha Demokrat.

Tuhuma hizi ni za karibuni kuliko zote zilizotolewa zikidai kuwa Russia iliingilia kati uchaguzi kinyume cha sheria.

Lengo la kampeni hizo chafu, mashtaka hayo yanasema, “ilikuwa kupanda mbegu ya chuki katika mfumo ya siasa za Marekani, ikiwemo uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.”

Tuhuma hizo zinahusisha njama, udanganyifu wa kifedha kwa kutumia mitandao na wizi wa vitambulisho kwa ujumla wake.

Mashtaka hayo yanatokana na uchunguzi uliofanywa na Mueller kuangalia jinsi Russia ilivyo ingilia kati uchaguzi na iwapo kulikuwa na mawasiliano kinyume cha sheria kati ya kampeni ya Trump na serikali ya Russia –Kremlin.

Kabla ya siku ya Ijumaa, watu wanne, akiwemo mshauri wa zamani wa usalama wa taifa na mwenyekiti wa zamani wa kampeni yake, walikuwa wamefunguliwa mashtaka na Mueller.

Hata hivyo ikulu ya White House haijatoa maelezo mara moja kujibu mashtaka hayo.

XS
SM
MD
LG