Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:15

Flynn akiri kuidanganya FBI


Michael Flynn
Michael Flynn

Mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Rais Donald Trump, Michael Flynn amekiri kusema uwongo Ijumaa alipohojiwa na wachunguzi wa idara ya upelelezi ya jinai ya Serikali Kuu (FBI).

Flynn ameiambia FBI juu ya mawasilianao yake na Russia wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais na alipochaguliwa kuwa mshauri wa usalama wa Trump.

Hatua hiyo inaashiria kwamba Flynn anatao ushirikiano na mwendesha mashtaka maalum wa serikali anaechunguza uwezekano wa Russia kuingilia kati uchaguzi wa Marekani 2016 na uwezekano wa kampeni ya Trump kushirikiana nao.

Flynn ameshitakiwa kwa kosa moja la kuwaambia uwongo wapelelezi wa idara ya uhalifu wa jinai FBI kuhusu mazungumzo ya faragha na balozi wa Russia nchini Marekani Sergey Kislyak.

Nyaraka ya mahakama iliyotolewa leo inaeleza mazungumzo yao yalilenga vikwazo vya marekani dhidi ya Russia vilivyowekwa na utawala wa rais Barack Obama.

Nyaraka hiyo, ambayo imesainiwa na mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller, imesema kuwa Januari, mara baada ya Trump kuapishwa, Flynn kwa hiari yake na kwa kujua alitoa nyaraka za uongo, kughushi na matamko ya uongo kwa wachunguzi juu ya mazungumzo yake na Kislyak.

Waendesha mashtaka wamedai kuwa Flynn aliwadanganya maafisa wa FBI Disemba 2016 kuwa hakumtaka Kislyak kujizuilia ili kuepusha kuongezeka kwa mgogoro huo baada ya Marekani kuweka vikwazo dhidi ya Russia siku ile ile.

XS
SM
MD
LG